"Indeed, truly, I shall enjoy
You are good, town of Amu
You have kind-hearted people
Whom I treasure dearly.

Their houses are adorned
They are truly beautiful
They possess abundant riches
I am proud of them too.

And the moon shines brightly
I follow tradition and custom
They are famous workers
Original inhabitants.

Yes, it has a sea
With beautiful horizons
Especially at dawn
Satisfying to behold.

Even when the sun sets
There's nothing to say
It doesn't trouble the heart
It's witnessed by all."

"Hakika kweli nitamu
Mui mwema hūnu Amu
Una watu makarimu
Walo nanjema twabiya.

Zaamu nyumba zadari
Zilo wakwa kwa uzuri
Mbwawaamu utajiri
Nifakhari yake piya.

Nao mui kunawiri
Nimila na dasturi
Zawakazi mashuhuri
Wenyeji waasiliya.

Naamu ina bahari
Yenye mema mandhari
Hususan alfajiri
Hushibi kuyangaliya.

Yuwa liwapo huzama
Hapo sina la kusema
Huiliwaza mitima
Yawenye kushuhudiya."
Lamu Poet Ustadh Mau